[Intro]
Mwishoni darasa la saba
Mimi na yeye ndo tulijuana
Sababu ya kukosa ada
Mimi na yeye ndo tulishindwana
[Verse 1]
Ndoto za udaktari kwisha habari
Zikapeperuka na yeye sekondari
Akahamishwa mbali mkoani Arusha
Hisia na balehe zilikuta nakata
Na ujana maji ya moto, eeh moyo mmoja
Basi nikaja kusikia yuko Gongo la Mboto
Mara chuo Mtwara, Masasi
Nyie wahenga waongo mara dunia ndogo
Mbona sijui sasa yuko wapi?
[Chorus]
Namtafuta, bado namtafuta
Mchumba wangu wa darasa la saba
Najua sikuchezea fursa
Ni wazazi walikosa ada
[Teree niee Teree sanam] x4
[Verse 2]
Mara ya mwisho kumuona
Ni siku ya mahafali
Niliandika ujumbe ila ye haukuusoma
Nyuma ya daftari
Suluhisho ni kupona nijue angali
Mzima yupo salama
Niache kusonona moyo upate afadhali
Nikimuona ntamsimulia
Yote niliyopitia ajue ye ndo chanzo
Cha mimi kuishi duniani
Nilivyommisi ntamkumbatia
Huenda naye kanimissi pia
Ni mawazo yanayonizunguka kichwani
[Pre-Chorus]
Ndoto za udaktari kwisha habari
Zikapeperuka na yeye sekondari
Akahami