[Intro]
Wema wa Mungu, uko nami daima, na nilipo fika kweli Mungu ni Ebeneza
[Verse 1]
Natazama nilikotoka, na mapito niliyo pitia, Mungu wa tusiyo yaweza, daima unaniongoza, uko na mimi wakati wote wa shida.
[Pri Chorus]
Bado nakutegemea uliye nivusha ng'ambo, kwenye giza na majaribu, wala sikua pekeyangu, najua umwema, hilo ndilo linalonivutia.
[Chorus]
Sauti zote zivume, zikuhimidi Mfalme, wema wako jina lako, lapita majina yote, Milimani zisikike, vilindini watambue, pendo lake Mfalme, linadumu siku zote Amina.
[Verse 2]
Mwangu moyoni tawala ndani yangu, pendoni mwako kuna furaha pia, Nakupenda Bwana nitabaki nawe daima.
[Pre Chorus]
Bwana ninaomba nuru za uso wako, hata niendako, niwe nawe Mungu, ongoza maisha, Na mimi nitakuimbia.
[Chorus]
Sauti zote zivume, zikuhimidi Mfalme, wema wako jina lako, lapita majina yote, Milimani zisikike, vilindini watambue, pendo lake Mfalme, linadumu siku zote Amina.
[Bridge]
Ulimwenguni kote Nuru itawale, waliona shida Bwana wote waokoe, nami nakupenda Mungu kwakua unanisikia.
[Chorus]
Sauti zote zivume, zikuhimidi Mfalme, wema wako jina lako, lapita majina yote, Milimani zisikike, vilindini watambue, pendo lake Mfalme, linadumu siku zote
[Outro]
Sauti zote zivume, zikuhimidi Mfalme, wema wako jina lako, lapita majina yote, Milimani zisikike, vilindini watambue, pendo lake Mfalme, linadumu siku zote Amina.