[Intro]
Nashangilia kwa amani, ndani ya giza napata mwanga
[Verse 1]
Nionapo amani kama shwari, au nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha, ni salama rohoni mwangu
Salama rohoni, ni salama rohoni mwangu
[Verse 2]
Ingawa shetani atanitesa, nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu, amekufa kwa roho yangu
Dhambi zangu zote, wala si nusu, zimewekwa msalabani
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu
[Chorus]
Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia
Utakaposhuka sitaogopa, ni salama rohoni mwangu
[Bridge]
Katika mateso na furaha, mimi ni salama rohoni mwangu
Hifadhi moyo wangu kwako, usiku na mchana
[Verse 3]
Salama rohoni, ni salama rohoni mwangu
Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia
[Outro]
Ninapoendelea kushikamana na imani, ni salama rohoni mwangu
Hakika nimeokolewa, salama rohoni mwangu