Nilikuwa gizani, bila tumaini
Dhambi zilinifunga, machozi moyoni
Yesu akaja, kwa upendo wake
Akanitoa huru, kwa damu yake
Nimegombolewa na Yesu
Niende tena kwa nani?
Amenipa uzima mpya
Niende tena kwa nani?
Nimegombolewa na Yesu
Mwokozi wa kweli
Hakuna jina lingine
Niende tena kwa nani?
Nilichoka kutangatanga
Kutafuta amani duniani
Lakini Yesu akaniita
Akanipa raha moyoni
Yesu, Yesu, wewe peke yako
Njia, kweli na uzima
Nitaishi kwa ajili yako
Leo na hata milele
Nimegombolewa na Yesu
Niende tena kwa nani? 🔥🙌
FAMILIYA YA MAYAGA TUNASHUKURU MUNGU