[Intro]
Furaha ni kuimba, sifa zake Jehova, Atukuzwe Muumba, aliyetukomboa.
[Verse 1]
Utukuzwe Jehova, wema wako twaona, Kila kunapo kucha, Mengi watushindia, daima twakwimbia, sifa zote pokea, utukuzwe Jehova, kwa uliyotutendea.
[Pre Chorus]
Utukuzwe jehova, kwa uliyotutendea.
[Chorus]
Fadhiri zako nitazitangaza, watu waone wema wako, na kinywa changu siwezi nyamaza, kulisifia jina lako.
[Verse 2]
Wewe Mungu Muumba, hilo twalitambua, ndio mana twaimba, sifa twakupatia, ndege nao waimbe, wanyama watambue, wewe Mungu Muumba, sifa zote pokea.
[Pre Chorus]
Utukuzwe jehova, kwa uliyotutendea.
[Chorus]
Fadhiri zako nitazitangaza, watu waone wema wako, na kinywa changu siwezi nyamaza, kulisifia jina lako.
[Bridge]
Tarumbeta yaimba, filimbi ya sikika, zeze inayopigwa, sifa kwako Jehova, watu wote waimbe, siku zote waseme, wewe Mungu Muumba, sifa zote pokea.
[Chorus]
Fadhiri zako nitazitangaza, watu waone wema wako, na kinywa changu siwezi nyamaza, kulisifia jina lako.
[Outro]
Fadhiri zako nitazitangaza, wote waone, pendo lako, na wema wako nitautangaza, wote wajue, waje kwako.