[Intro]
[Verse 1]
Elisha Juliasi nimeona niimbe wimbo huu,
Ili kila mtu asikie sauti ya onyo.
Dunia imejaa giza na udanganyifu mwingi,
Lakini Bwana bado anaita watu watubu.
Wanaovaa suluali bila aibu mbele za Mungu,
Na wanaovaa vimini hata kanisani,
Wanaovaa mpasuo mpaka makalioni ,
Wasipotubu njia yao ina ishia motoni.
[Chorus]
Wanaenda motoni wote,
Wanaenda motoni.
Wanaenda motoni wote,
Wanaenda motoni.
[Verse 2]
Wengine wanajiita mishangazi Kwa watoto wadogo
Lakini maisha yao hayampendezi Mungu.
Manabii feki nao wamejaa duniani,
Wanapotosha watu kwa tamaa ya mali.
Wanauza mafuta ya kupikia wakisema ni upako,
Wanauza udongo wakisema ni wa Israeli.
Lakini kweli ya Mungu haisaidii kwa biashara,
Wanaochezea jina la Bwana wanaenda motoni.
[Chorus]
Wanaenda motoni wote,
Wanaenda motoni.
Wanaenda motoni wote,
Wanaenda motoni.
[Bridge]
Tubuni watu wa Mungu kabla mlango haujafungwa,
Yesu bado anaita, njoo urudi nyumbani.
Acha dhambi, shika njia ya wokovu,
Ili siku ya mwisho usiende motoni.
Acheni kuuza miliyenu nyie mabinti mna ena motoni
Acheni watoto wa elfumbili wana wapeleka motoni
Wakezawatu Wana wapeleka motoni badilikeni msiishie motoni