Kweli mkataa pema pabaya panamwita
Nyangeta mtoto wa Mwita, alikuwa mtata
Siku zikapita Nyangeta anakula bata
Hata umwambie nini takataa katakata
Hii ni story, ya yule shori binti mtoto wa tajiri
Nami naileta kwenu iwafundishe maadili
Alizaliwa peke kwenye familia yake
Mtoto wa kike matajiri wazazi wake
Baba wakili mama mbunge mahiri
Alizaliwa kwenye nchi ya maziwa na asali
Miaka ikasogea binti naye akakua
Akilelewa vyema na dada wa kazi Maua
Alipendwa sana Nyangeta mi nakwambia
Kila alichotaka wazazi walimletea
Midoli matoi na mabembea pia
Mapiza na mabaga na mabagiabagia
Myaka sita ikafika, umri mwafaka
Wazazi hawakusita shuleni wakampeleka
Ili apate elimu mtoto wa kiafrika
Ndio urithi muhimu wa baadae ni uhakika
Nyangeta bwana akaanza chekechea
Akapambanapambana la saba akatoboa
Wakafurahi wazazi wote wawili
Kwamba Nyangeta sasa anakwenda sekondari
Kilichofata sekondari ni hatari
Wacha nipoze koo subiri vesi ya pili
Ahaa, kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa
Tunaposhiba tusijisahau kuna njaa
Ahaa, kiburi ni balaa ukiheshimu watu kamwe hutalala njaa
Ahaa, kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa
Tunaposhiba tusijisahau kuna njaa
Ahaa, kiburi ni balaa ukiheshimu watu kamwe hutalala njaa
Sekondari ya bweni alianza vizuri
Siku zilivyopita akaanza ujeuri
sababu ya utajiri, wa baba na mama
Akabweteka akazembea kusoma
Mana alipewa nyingi pesa za matumizi
Pesa iliwekwa benki kila mwisho wa mwezi
Akapata rafiki aliyeitwa Sara
Mtoto wa meneja wa benki ya biashara
Walitoroka shule wakaenda viwanja
Walimu wote wanoko walipewa mikwanja
Wakakausha, ikawa ndo maisha
Hivyo kila wikiendi walikwenda kujirusha
Siku zakapita miaka ikasogea
Hatimaye kidato cha nne akaingia
Hali ikawa mbaya akawa mshenzi wa tabia
Malaya, mlevi na mvuta bangi pia
Isivyo bahati Nyangeta akapata mimba
Akaacha shule maskani akatinga
Wazazi wake wakakata tamaa
Nyumbani akakaa, mtoto akamlea
Jeuri yake fedha za baba na mama
Ya Mungu mengi waswahili wanasema
Unajua nini, balaa likatokea
Baki hapo siondoke nakuja