Nimeelwa (Couplet 1)
Ya kwamba ni wewe Yesu
Uliyenitunza, nilipoumwa
Nimeelewa, ya kwamba si kila mtu
Ninayepaswa, elezea shida zangu
Wewe ni Mungu wangu, wewe
Nimeelewa ya kwamba ninapoumwa
Ni wewe ambaye, unanitibu
(Refrain)
Ewe Mungu wangu ninakuomba, unirehemu
Kwa sababu wewe Mungu
Nimeelewa, ya kwamba ni wewe Yesu
Uliyenitunza, nilipoumwa
(Couplet 2)
Mara nyingi sisi wanadamu tunasahau
Makuu yako, unayoyatenda
Nimeelewa, ni wewe mpendwa wetu
Unayeyetulinda, kwa hali yoyote
Nimeelewa umetulinda wewe Mwokozi
Unatenda mambo, ambayo mwanadamu hawezi
(Pont - Gratitude)
Inakushukuru Yesu, kwa sababu Mwokozi
Unatenda mambo, ambayo sisi hatuwezi
Na mara nyingi, matatizo yakiwa mengi twajiuliza
Ni kwa nini hivi?
Shida zimekuwa nyingi sana, hatujui mwisho ni gani
Ila twakuamini wewe ushikaye mambo
Tunatia vyote mikononi, Mwokozi
Tukijua ya kwamba utatulinda sisi
(Message d'encouragement)
Ewe ndugu yangu, unayekata tamaa
Ninakuambia, ujipe moyo
Mimi ninakuambia, ujipe moyo ndugu yangu
Kwa sababu maisha haya, hayatadumu pia
Na kuna maisha, baada ya haya ya hapa duniani
Mpendwa wetu...
(Outro)
Mimi Volonte Bahati, nimetambua ya kwamba
Si kila mtu, apaswa jua siri zako
Mimi Volonte Bahati, ninayemba nina imani
Nikiamini ya kwamba atatulinda sisi
Kesho inanitia hofu, sijui inabeba nini
Ila namwamini yeye aishikaye kesho.