Mshika mawili moko huponyoka
Ukimpenda john usimpende na dula
Maana Binadamu
hatuna moyo wa chuma
Ukimpenda fatuma
usione ni suna
Ingawa...
Tumeumbiwa hisia,kupenda lazima
Ila Sometimes, zinapoteza mazima
Tatizo macho hayataki kuona
Kila kipitacho kwake kimenona
Iwe hadharani ama kwenye kona
Lazima moyo kuuponza
Pre chorus
Mwenzioo nina familia
na nina watu wananitegemea
Hizo tabia moyo achilia
za kupenda penda kila anae kufatilia
Punguza sifa maana utajifia
hawakupendi wanakutumia
Tulia tulia (akupendae una muumiza)
Tulia tulia (akupendae utampoteza)
Tulia tulia (tamaa mbaya inaponza)
Tulia tulia (moyo wangapi utawapenda)
tulia hheeee tuliaaa mpenzi wangu nampenda
Nakuomba tuliaaa uuhhh uuhh tuliaaa eeh
Verse 2
Cha mtu sumu
Ila kulusumu
Yeye haogopi kunipa vitamu
Kila muda akienda akirudi
Habishi hodi anaingia hadi ndani
Huku si ndo kuwekana matatani
Maana anajua lazima nitakubali
Sababu sumaku hainasi majani eeh
Pia na roda ndugu yake swaumu
Kila akiniona ana vaa nguo za humu
Ili kwake ni nase moyo niulaumu eh
Pre chorus
Mwenzioo nina familia
na nina watu wananitegemea
Hizo tabia moyo achilia
za kupenda penda kila anae kufatilia
Punguza sifa maana utajifia
hawakupendi wanakutumia
Tulia tulia (akupendae una muumiza)
Tulia tulia (akupendae utampoteza)
Tulia tulia (tamaa mbaya inaponza)
Tulia tulia (moyo wangapi utawapenda)
tulia hheeee tuliaaa mpenzi wangu nampenda
Nakuomba tuliaaa uuhhh uuhh tuliaaa eeh
Bridge
Tamaa ziweke mbali
Anaekupenda usimuachilie
Mwili hulagai
Anaekupenda mng'ang'anie
Final chorus
Tulia tulia tulia na akupendae
Tulia tulia usije juta baadae
Nasema tulia tulia na akupendae
Tulia usije juta baadae
Outro
Baba nancy asante kwa kutunga