1. Siku moja mavuno yataisha kabisa, baada ya hayo
hukumu. Jua litazimika siku hiyo ya mwisho, na
hutasikia injili.
Atakusanya ngano kwa furaha ghalani, bali
makapi yote yatatupwa motoni. Rafiki,
utakuwa wapi?
2. Mahubiri na nyimbo za wokovu wa Mungu
zitakaponyamanza huku, uliyelikataa neno zuri la
Mungu, utakaa wapi milele?
3. Watu wote wa Mungu wafikapo mbinguni kukaa
pamoja na Yesu, wataimba kabisa kwa sauti ya
nguvu kumshangilia Mwokozi.