Rafiki yangu alinambia kwamba
Amekata tamaa, amevunjika moyo
Yalomkuta yamemlamba chenga yamempiga kanzu na tobo juu
Maisha yamekuwa magumu
Na hajui afanye nini, oooh!
Wala ashike lipi oooh!
Anatamani kuwa mwenye furaha kama wengine, kama wengine
Lakini pesa inavyomkataa hana kingine cha kufanya aishi kwa raha
Aaaaa, ana majonzi ana huzuni tele analia
Aaaaa, anatamani kuishi kwa furaha lakini da!
Aaaaa, ana majonzi ana huzuni tele analia
Aaaaa, anatamani kuishi kwa furaha lakini basi ndo hivyo tena
Nikamwambia rafiki yangu kaa chini
Nisikilize msela wangu kaa chini
Unaniona mimi, nimevaa vizuri
Nimependeza na ninanesanesa
Usoni mwangu nimenawiri aaah
Na nina uso wa ujasiri aaah
Majanga yako si mengi kuliko yangu
Watu wa benki wanataka uza nyumba yangu
Nina mkopo nimeshindwa kulipa
Usinione ndugu yangu niko hapa
Huko shuleni walimu wananikaba
Ni siku tatu nimepewa nilipe ada
Ule ugonjwa wa mamangu umerejea tena unahitaji pesa daa,
Ndo hivyo tena na mimi ndo baba wananitazama nitafanyaje sasa daa,
Hapo mgonjwa kageuka muuguzi
Rafiki yangu sasa akamwaga machozi
Akanihurumia akanambia pole eeeeh!
Aaaaa, kumbe maisha ndivyo yalivyo bwana wee!
Aaaaa, kila kiumbe ana msalaba wake ee!
Aaaaa, kumbe maisha ndivyo yalivyo bwana wee!
Aaaaa, kila kiumbe ana msalaba wake ee!
Wewe unayeyapitia magumu usilie
Kaza moyo bwana
Usiwaze wala kunywa sumu usilie kaza moyo bwana
Pambana tu, yale unayoweza yafanye ee,
Unayoyashindwa mwachie Mungu
Ukikosa usitukane ee, huenda kesho ndo lako fungu
Mapambano hayana mwisho, pambana
Wala hayana mwisho kazana
Ndugu huenda kesho, kazana
Mahangaiko yakawa mwisho