Naanza na kusema asante kwako mungu...
Binadamu walinipa ukilema ila wewe ukanipa mwendo..
Basi nami sioni tena haya ya kukusifu na kukuabudu..
Nitakuabudu siku zote za maisha yangu ulionipa
Niko na maadui hata wengine siwajui wala sikuwa kosea ila Ombi lao kwangu niwaone nime yapoteza maisha yangu.. Nakupa sifa zote na wacha sifa zikuwendee
Maana unanishangaza nalala tahira naamka mzima
Nahisi hii ni njia ya watu wajue kweli mungu yupo
Nilindie wanao nijali na uwape maisha marefu
Babangu na mamangu ndugu zangu Nilindie mungu sitasahau hata rafiki wanao ni shika mkono pia wakumbuka.. Leo naja mbele zako mdhaifu na mchovu nilicho baki nacho tu ni imani kuwa utanihinua na kunifariji
Wadunia yang'ang'ana kuniaribu akili kwa maneno.. Ila nami naiumba akili yangu tena kwa maombi na imani kwako
Ombi langu kwako jionyeshe ndani yangu mola walio mpiga chura teke wajue ilikuwa kuvusha mto Wa shida... Leo nimejua mungu hupo na ufanani na binadamu wacha sifa zikurudie mungu... Kwani pangapi nimefukuzwa kwale mombasa na kwingi ilanina imani utanipa makao ya furaha na amani tena
Watu wame nipa ujasiri bila kujua maana wamefanya nijuwe naweza maana wana jikusanya kunipa majina tahira chizi ila cha ajabu wanapo niona wanashindwa maana unanijenga kifahamu na kunipa moyo zaidi siwezi kujishindanisha na watu wanao nikataa ila ninaimani utanipa ushindi machoni mwao wajuwe kweli upo.. Upo mda najiuliza mimi ni nani maana napo jawa na hofu naona vua kama jibu langu basi wacha baraka zangu ziwe mvua maishani mwangu... Leo naiita mvua kwa jina lako kuuonyesha ulimwengu kuwa upo na una weza
Nipe moyo kwa kipindi hiki kigumu mungu
Nipe tena ujasiri ewe mungu... Wacha ning'ang'ane maana kupitia nija lako naweza... Basi ewe mungu nenda uyafanye madhaifu yangu daraja la mafanikio na unipe maisha marefu zaidi duini ya kulitangaza jina lako na wema wako asante asante asante jehova nime amini kweli upo na ni kweli upo