INTRO
Scarter Son… yeah
Scatter soni
Hao… hao… hao…
VERSE
Walisema wakina Salima,
Kila ninakopita me nafanya wanasimama wimamaneno,
Nikipita macho yanatoka kama sinema
Mitaani pressure naipima,
Nimekaza roho sikubali kudidimia,
Nimechoka kuomba heshima,
Sasa jina langu linajitambulisha lenyewe bila shida
INTER-CHORUS
Sina shobo na pesa zao, sina shobo
Na dada zao nami sishindani nao, bro
Nak’wetu nao na kwao wanashindwa
Vita zao nami sishindani nao
(Hao… hao… hao…)
CHORUS
Mugunghwa kkochi pieot seumnida
Nimesimama imara hata dhoruba ikija
Mugunghwa kkochi pieot seumnida
Mizizi iko chini, matawi juu angani yaenda
VERSE
Licha ya kuwa wananichukia, aah
Lakini hawaishi kunifuatilia, yeah
Nami sichoki, najipigania
That is cause I’m here, I’m here, here, here, here
Nilianza chini bila msaada
Leo nikihema tu, wanabadilisha mada
Nimepanda ngazi bila janja
Roho safi, akili kali, bado niko rada
CHORUS
Mugunghwa kkochi pieot seumnida
Muda ni mwalimu, nimefaulu somo zima
Mugunghwa kkochi pieot seumnida
Nipo hai, nipo kweli, nipo ndani ya jina
VERSE
Nilikaa kimya, nikajifunza sauti
Leo nikiongea, maneno yanapiga risasi
Hawanijui lakini wanani-hate bure
Wananitaja jina kama wanani-promote bure
Nimepita giza bila taa
Ndoto mkononi, jasho likiwa ada
Kila tone damu lilikuwa dua
Leo mafanikio yananitaja kama ndugu wa karibu, aah