*Titre : Nishike Mkono*
*Couplet 1 - ombi langu*
Nishike mkono Bwana, ukiniacha nitazama,
Mwenyewe sitaweza, nahitaji msaada wako.
Usinyamaze, ukiniachia nitapotea.
*Refrain - Hadithi ya Petro*
Siku moja Yesu akiwa karibu na wanafunzi wake,
Alitembea juu ya bahari.
Alafu mwanafunzi mmoja Petro alimwambia:
"Kama ni Wewe Bwana, niruhusu nami nitembee juu ya maji."
Yesu akamwambia: "Njoo."
Alafu Petro akaanza kutembea juu ya maji,
Lakini alipoona upepo na dhoruba, akaanza kuogopa,
Naye akaanza kuzama baharini.
Sababu alikuwa na imani ndogo,
Na hii ilisababisha woga na mashaka.
*Couplet 2 - Maungamo*
Na mimi ni kama Petro, nahitaji msaada wako Bwana.
Nishike mkono, imani yangu ni ndogo, ukiniacha nitazama.
Chunga roho yangu Bwana, maana safari ni ndefu.
*Pont - Tamko la imani*
Upepo, dhoruba vinapokuja nibaki imara,
Nakutegemea Wewe.
Usiniache Mungu wangu kupata haya, majaribu ni mengi hapa duniani.
Bila Wewe sitaweza.
Nipe mwisho mzuri kuliko mwanzo.
_Nakuhitaji Bwana!_
*Refrain Final
Nishike mkono, nisizame,
Nishike mkono, uniongoze,
Imani yangu ni ndogo, lakini Wewe ni Mkuu.
Nishike mkono Bwana, mpaka mwisho.