[Intro]
Wema wa Mungu, uko nami daima
[Verse 1]
Hatua niliyo fika kweli Mungu ni Ebeneza, (mana ni) Natazama nilikotoka, na mapito niliyo pitia, Mungu wa tusiyo yaweza, daima unaniongoza, uko na mimi wakati wa shida.
[Pri Chorus]
Bado nakutegemea uliye nivusha ng'ambo, kwenye giza na majaribu, wala sikua pekeyangu, najua umwema, hilo ndilo linalonivutia.
[Chorus]
Sauti zote zivume, zikuhimidi Mfalme, wema wako jina lako, lapita majina yote, Milimani zisikike, vilindini watambue, pendo lako e Mfalme, linadumu siku zote Amina.
[Verse 2]
Mwangu moyoni itawale amani, Mwako pendoni nimebaki, Mungu yu karibu nami, kuliko ninavyo dhani, Nakupenda wangu Mwokozi.
[Pre Chorus]
Bwana ninaomba nuru za uso wako, popote niendako, niwe mikononi mwako, ongoza maisha, Na mimi nitakuimbia daima.
[Chorus]
Sauti zote zivume, zikuhimidi Mfalme, wema wako jina lako, lapita majina yote, Milimani zisikike, vilindini watambue, pendo lako e Mfalme, linadumu siku zote Amina.
[Bridge]
Ulimwenguni kote Nuru yako na itawale, Uwe na wenye shida, kwa mapito waliyo pitia, Mungu wa tusiyo yaweza, sikia wanaokuomba, Wakumbuke wakati wa shida.
[Chorus]
Sauti zote zivume, zikuhimidi Mfalme, wema wako jina lako, lapita majina yote, Milimani zisikike, vilindini watambue, pendo lako e Mfalme, linadumu siku zote
[Outro]
Sauti zote zivume, zikuhimidi Mfalme, wema wako jina lako, lapita majina yote, Milimani zisikike, vilindini watambue, pendo lako e Mfalme, linadumu siku zote Amina.