[Intro]
Usiogope rafiki, neema ya Bwana iko nasi, katika taabu zote, ameahidi atakua nasi
[Verse 1]
Kitu gani kinachokutaabisha, Moyoni mwako umepoteza amani, (lakini pia) Maswali mengi unayojiuliza, ni ipi hatima ya maisha yako, (ndugu sikia) Kumbuka Yesu alivyotuambia "Njoni ,kwangu enyi nyote msumbukao" Tumtwike yeye fadhaa zetu zote za maisha.
[Pre Chorus]
Tukufuate wewe, Yesu faraja yetu, ya maisha
[Chorus]
Tazama Mungu yu mwema, Siku zote anatupigania, anatutetea Mungu, Mwingi wa Rehema, Moyo na umtukuze Bwana, siku zote yeye ni mwema, kila tukiomba Mungu anatusikia
[Verse 2]
Yesu mwokozi rafiki wa huruma, Tunabarikiwa sana kwa wema wako, (lakini pia) Wakati wote tunakutegemea mwokozi wetu na hatuna mwingine, Hata marafiki tunawaambia twende kwake Mwozi tupate uzima, Tukufuate wewe Yesu uliye Ngome ya uzima.
[Pre Chorus]
Tukufuate wewe, Yesu faraja yetu, ya maisha
[Chorus]
Tazama Mungu yu mwema, Siku zote anatupigania, anatutetea Mungu, Mwingi wa Rehema, Moyo na umtukuze Bwana, siku zote yeye ni mwema, kila tukiomba Mungu anatusikia
[Bridge]
Neema kubwa uliyotupatia, moyoni mwetu tunakutukuza Bwana, kwa furaha nyingi tunakuimbia, Mwokozi wetu na hatuna mwingine, nyakati zote unatupigania, Mungu wetu rafiki wa ajabu sana, tukufuate wewe rafiki yetu mwema wa maisha.
[Chorus]
Tazama Mungu yu mwema, Siku zote anatupigania, anatutetea Mungu, Mwingi wa Rehema, Moyo na umtukuze Bwana, siku zote yeye ni mwema, kila tukiomba Mungu anatusikia.
[Outro]
Utukuzwe Bwana, wema wako ni mkuu, mioyo yetu yakuhimidi, jina lako ni kuu.