Only you my God, WE love you for all
Kwani wewe ndiyo unaendeleya kutuchunga
Hata nikitembea bondeni mwa uvuli wa mauti
Nahisi mkono wako, unaniambia nisimame, siwe mnyonge
Ulinichora kwenye kiganja chako, huwezi kusahau
Kila pumzi naipiga ni zawadi kutoka kwako
Nilikua sifuri, ukaniita mfalme
Nilikua mtumwa wa dhambi, ukalipa fidia yangu
Msalabani pale Golgotha, damu ikamwagika
Kwa ajili yangu mimi, ili nipate uzima
Only You my God, no one else above You
Kwani wewe ndiyo unanipeleka mbele
Only You my God, You’re the reason I’m breathing
Uwezo wako Mungu, hauna mipaka
Ma-doctor wakisema hapana, Wewe unasema ndiyo
Milango ikifungwa, Wewe unafungua njia mpya
Hakuna mlima hauwezi kuubomoa
Hakuna tatizo hauwezi kulitatua
So natupa mikono juu, nakiri Wewe ni Mungu
Mkubwa, mwema, mwaminifu, wa milele