MUNGU AWABARIKI MAMANGU FAZILAH NA PAPA DELEGUE MUSUBAO
Katika Jina la Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai,
Tunamsifu Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.
WaKristo wote wa Makeke,
Nawasalimu katika Jina takatifu la Yesu Kristo.
Kanisa letu la Anglicane Makeke,
Bwana awabariki na awaongezee neema.
Leo tunaimba si kwa sababu ya utajiri,
Si kwa sababu ya mali ya dunia,
Bali kwa sababu Mungu ametutendea mema.
Wimbo huu ni sadaka ya shukrani,
Kwa wazazi wetu wapendwa:
Mama Kavugho-Mutwikalo Fazilah
Na
Papa Kambale-Musubao Efrem Délégué.
Utukufu wote ni wa Yesu Kristo.
Mungu aliwaunganisha kwa upendo wake,
Akawajalia moyo wa uvumilivu.
Mkajenga nyumba juu ya Mwamba ulio imara,
Mkafundisha watoto njia ya Bwana.
Kwa maombi yenu,
Familia ilisimama.
Kwa machozi yenu,
Mungu alifungua njia.
Kwa imani yenu,
Vizazi vinaendelea kumwabudu Kristo.
Leo tunasema:
"Asante Yesu..."
*<<Mungu awabariki Mama KAVUGHO FAZILAH na Papa KAMBALE DELEGUE,*
*Awape afya na maisha marefu.*
*Awainue katika mipango yao yote.*
*Amani ya Kristo ikae ndani ya nyumba yao.*
*Familia yao izidi kumtukuza Yesu Kristo .*
*Yesu ndiye Mwanzo.*
*Yesu ndiye Mwisho.*
*Yesu ndiye Tumaini letu milele.>>*
Bwana akaibariki familia hii kwa watoto wa dhamani kama:
*PALUKU-MANZEKELE Fiston,* mzaliwa wa kwanza,
Bwana akufanye nguzo ya imani,
Uwe mtumishi mwaminifu wa Kristo.
KAHINDO NEÉMA ALEXANDRINE,
Neema ya Mungu ikufunike kila siku,
Maisha yako yawe ushuhuda wa upendo wa Yesu.
GLORIA ALEXANDRINE
Utukufu wa Mungu uangaze ndani yako,
Wengi wamjue Kristo kupitia maisha yako.
HEKIMA MANZEKELE
Tembea katika hekima itokayo juu,
Roho Mtakatifu akuongoze katika kila hatua.
CHADRACK MANZEKELE, hawa niwamapacha na Mechack, CHADRACK
Simama imara katika imani,
Usiogope majaribu,
Kwa maana Mungu yu pamoja nawe, Sasa
MECHACK MANZEKELE,
Ingawa ulitangulia mbele za Bwana,
Tumaini letu linabaki ndani ya Kristo,
Tutakutana tena siku ya utukufu.
USHINDI MANZEKELE,
Ushindi wako uwe ndani ya Yesu Kristo,
M IT