Intro
Yeah....shadrack...mtafutaji wa kweli....wengine uandika kwa kalamu,mimi naandika kwa machozi....
Verse1
Nimeamka asubuhi jua bado halija chomoza, mama anahema,kabati halina hata mahindi ya kusonga.
Baba ametoka jana hajarejea,
Anatafuta mkate mtaani,bila mwelekeo wala njia.
Sina viatu, lakini nina ndoto kubwa,
Za kuinua familia,sio tu kuvaa nguo mpya.
Shule naenda kwa miguu, moyo wangu ukisali,
Mwalimu anafundisha future, mimi nawaza chakula cha jioni hali.
Wenzangu wanazungumzia TIKTOK na filters, mimi nawaza gharama ya daftari na changamoto za sisters.
Kila mtu ana mitihani, hata isiyo andikwa darasani,
Maisha ni kama somo,usipojifunza unaanguaka kisayansi.
Hook
Maisha ni mitihani hila si kila mtihani wa kuogopa .
Kuna waliofeli jana,leo ni viongozi wetu na tena kwa bidii na subira zao.
Usikate tamaa ndugu,majibu yapo ndani yako , ukiamini unaweza -hakuna mtihani utakaoshindwa.
Verse 2
Niliona mzee mmoja, mwalimu aliyekufa masikini
Alifundisha hekima,lakini hakujifunza kudaai haki.
Dada mmoja anauza vitumbua na ndoto zake mkononi,
Ana stashahada mfukoni,lakini mtaani hakuna hajira ya milioni.
Rafiki yangu alikata tamaa, akasema maisha si hali,
Nikamwambia "Bro,hata samaki hupambana dhidi ya maji."
Mitihani ya maisha haiji na karatasi na kalamu,
Inakuja na vilio,vizingiti ,n sauti ya ndani ikisema *endelea shad........usikate tamaa*
Hook inayorudia kwa nguvu
Maisha ni mitihani-ila si kila mtihani wakuogopa,
Kuna waliofeli jana, leo ni viongozi wa kesho kwa bidii na subira.
Usikate tamaa ndugu,majibu yapo ndani yako,ukiamini unaweza-hakuna mtihani utakaoshindwa"
Outro
"Majibu yako hayapo kwenye kitabu cha mtu mwingine........
Yapo ndani yako. Jitambue yeah jifunze.uendeleee