Siku ya tatu sijakuona, na nimekonda
eti mamy ni kweli ulinipenda?
maana nahenya na nahangaika kama bwege
umesepa na asali na umeniachia masege
rudi nyumbani natamani kukuona
tujenge familia na maradhi nitapona
amini we pekee nakupenda, umekwenda
hebu nicheki kwanza nilivyokonda
nakumbuka zamani, ilitawala amani
mbona siamini ni kama niko ndotoni
katika kupambanapambana tulikwazana
tukaumizana, tukalizana
hasira zikatawala na tukapotezana
da, nisamehe mpenzi wangu
ni kwasababu yangu pametokea ukungu
ukaleta machungu, namuomba Mungu
akupe moyo mwema hatimaye urudi kwangu
kama bahati nilikupata kimwali, binti mkali nikajidai kiukweli
nilitamba na wewe kila tulipokwenda
madenda, yaliwatoka hadi wapemba
ooh ma Gad, sijui zitakuwa lini
siku nzuri kama zile za zamani
ahaaaa, rudi kwangu mamaa nihurumie
ahaaaa, nakupenda sanaa unielewe
ahaaaa, rudi kwangu mamaa nihurumie
ahaaaa, nakupenda sanaa unielewe
wangu kipenzi, mwerezi na mjuzi
ninakupenda sana na kukuacha siwezi
nilikuwa mshenzi, mwizi na mpuuzi
nilirukaruka mitaani na mamanzi
sasa nimerudi, kwako na magoti
nifinyefinye sana, nitandike makofi
na, ukimaliza nisamehe nipokee
tufurahi pamoja na tufanye sherehe
kama ningeweza kurudisha siku nyuma
ningefanya kila kitu, ili niwe mwema
mashemeji zako maskani wanauliza
wapi shemeji nabaki tu najibaraguza
sikia mamy, sina jingine mimi
nimeshalia sana ninaomba uniamini
nimebadilika na nimejifunza pia
amini, ule upuzi sitarudia
ahaaaa, rudi kwangu mamaa nihurumie
ahaaaa, nakupenda sanaa unielewe
ahaaaa, rudi kwangu mamaa nihurumie
ahaaaa, nakupenda sanaa unielewe
oy, sikia mrembo, shemela
acha kukaza shingo, msamehe msela
ona analia, na unamsikia
punguza kumkazia mwana ameshajutia
maskani pamepoa kinoma mi nakwambia
yote sababu yako kimwana sasa sikia
sisi tumeshakaa, tumemsema masaa
ameshabadilika ninakuhakikishia, aah!
na mwaka huu tunavuta jiko sawa?
we usikwame timba geto kama kawa
geto fagia, fua nguo anua
na wana tukitimba misosi pika pakua
tutakulinda shem tutakute