[Intro]
Kwa mkono wako bwana, sisi tuko salama
[Verse 1]
Maumivu makali aliyo pewa, Mwokozi wa maisha yetu, hata leo ninafikiria mimi ni chanzo cha yote,
Alipigwa mwokozi yesu, alibeba huzuni zetu, alihakikisha, analilipia, deni lote lisije kwetu,
[Pre-Chorus]
Alihakikisha analilipia deni lote lisije kwetu
[Chorus]
Aliacha kiti cha enzi, akaja kufa juu ya msalaba,
Kwa dhambi zetu aibu yetu, kwakweli yesu alitubeba, Maumivu makali aliyopewa, yalifanya mi na wewe tumepona, ikumbukwe, tukiasi, tunamrudisha juu ya msalaba, Maumivu makali aliyo pewa, yalifanya me na wewe tumepona, ikumbukwe, tukiasi, tunamrudisha juu ya msalaba
[Verse 2]
Niukweli mi na wewe tumepona, kwa damu yake bwana yesu, neno lake linatuambia, tusitende dhambi tena, na tujisalimishe kwake, yeye pekee atuongoze, nia zetu na mawazote yetu, yeye pekee atuongoze,
[Pre-Chorus]
Nia zetu na mawazote yetu, yeye pekee atuongoze
[Chorus]
Aliacha kiti enzi, akaja kufa juu ya msalaba, Kwa dhambi zetu aibu yetu, kwakweli yesu alitubeba, Maumivu makali aliyopewa, yalifanya mi na wewe tumepona, ikumbukwe, tukiasi, tunamrudisha juu ya msalaba, maumivu makali aliyo pewa, yalifanya me na wewe tumepona, ikumbukwe, tukiasi, tunamrudisha juu ya msalaba
[Bridge]
Wema wa Mungu dhahiri tumeuona, akiwa na maisha yetu, mambo mengi anatutendea, hayahesabiki kamwe, Pendo lake ni la milele, wema ndiyo tabia yake, ni hakika bila pendo lake tungeangamia milele
[Chorus]
Aliacha kiti enzi, akaja kufa juu ya msalaba, Kwa dhambi zetu aibu yetu, kwakweli yesu alitubeba, Maumivu makali aliyopewa, yalifanya mi na wewe tumepona, ikumbukwe, tukiasi, tunamrudisha juu ya msalaba, maumivu makali aliyo pewa, yalifanya me na wewe tumepona, ikumbukwe, tukiasi, tunamrudisha juu ya msalaba
[Outro]
Hallelujah msifuni bwana, maana fadhiri zake ni za milele, viumbe wote na washangilie, fadhiri za bwana zadumu milele Amen