[Intro]
Upendo wake yesu, ni mkuu sana, neema yake kwetu ni ya pekee
[Verse 1]
Habari ya ukombozi wetu sisi wanadamu ina maajabu, kuacha enzi juu mbinguni kuja mpaka dunia kwa ajili yetu,
Pendo lake Bwana yesu juu ya maisha yetu lina maajabu, kubeba zote dhambi zetu, kuteswa hata mauti kwa ajili yetu
[Pre Chorus]
Wema wa ajabu juu yetu, kutoka mbinguni kuja kwetu,
Ni ajabu pendo lake kwetu, kujitoa kubeba taabu
[Chorus]
Ni upendo wa ajabu, ni upendo wa ajabu, kuacha enzi juu mbinguni kuja mpaka duniani kwa ajili yetu.
Ni upendo wa ajabu, ni upendo wa ajabu, kuacha enzi juu mbinguni kuja mpaka duniani kwa ajili yetu
[Verse 2] Kifo juu msalabani tena bila ya hatia nayo ni ajabu, kutenda mingi miujiza na bado wasiamini nayo ni ajabu,
Yesu kwetu ni rafiki kukataa wema wake nayo ni ajabu, kupenda dhambi na dunia kuliko wema wa mungu nayo ni ajabu
[Pre Chorus]
Kwakweli ajabu ya neema, kujito kwa ajili yetu, pendo lake, linatushangaza, kujitoa kwa ajili yetu
[Chorus]
Ni upendo wa ajabu, ni upendo wa ajabu, kuacha enzi juu mbinguni kuja mpaka duniani kwa ajili yetu.
Ni upendo wa ajabu, ni upendo wa ajabu, kuacha enzi juu mbinguni kuja mpaka duniani kwa ajili yetu
[Bridge] Mwokozi yesu samehe dhambi zetu, takasa moyo osha nia zetu, tusafishe kwa damu ya neema, tuongoze na utuokoe,
Shauku yetu tukuone wewe, akili zetu zikuwaze wewe, na njia zetu tutembee nawe, milele yote tuongoze wewe
[Chorus]
Ni upendo wa ajabu, ni upendo wa ajabu, kuacha enzi juu mbinguni kuja mpaka duniani kwa ajili yetu.
Ni upendo wa ajabu, ni upendo wa ajabu, kuacha enzi juu mbinguni kuja mpaka duniani kwa ajili yetu
[Outro]
Utukuzwe sana Mungu wetu, pendo kuu sana juu yetu, mwanga wa mbingu tumaini letu, heshima zote zije kwako yesu